Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 43 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 561 2023-06-08

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -

Je, lini Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro itakuwa Jiji?

Name

Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, uanzishaji au upandishaji hadhi wa Halmashauri upo kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 287 na 288 pamoja na Mwongozo wa uanzishwaji wa Maeneo ya Utawala wa Mwaka 2014.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI haijapokea kusudio la kupandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuwa Halmashauri ya Jiji. Hivyo kwa sasa Serikali imeweka utaratibu katika kuimarisha miundombinu ya huduma za jamii kwa maendeleo yaliyopo kabla ya kuanzisha mamlaka mpya za utawala.