Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 42 Finance and Planning Wizara ya Fedha na Mipango 549 2023-06-07

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. CECIL D. MWAMBE K.n.y. MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza:-

Je, lini Benki ya CRDB itafungua tawi katika Mji wa Mangaka?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahya Ally Mhata, Mbunge wa Nanyumbu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Benki ya CRDB imeanza ujenzi wa tawi katika Mji wa Mangaka. Tawi hilo linatarajiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa mji huo kabla ya mwezi Septemba 2023, ahsante.