Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 40 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 522 2023-06-05

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza: -

Je, ni lini minara ya simu itajengwa maeneo ya Endahagichang, Tumati Juu, Qalodaginwe, Aidurdagawa, Qamtananat na Migwa?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA NA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Endahagichang imeingizwa katika mpango wa kufikisha huduma ya mawasiliano kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali, ambapo vijiji vitakavyonufaika ni Endadubu, Miqaw na Endahagichan.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itafanya tathmini katika maeneo mapya yaliyowasilishwa na Mheshimiwa Mbunge ambayo ni Tumati Juu, Qalodaginwe, Aidurdagawa, Qamtananat na Miqaw ili kubaini changamoto za huduma za mawasiliano zilizopo.