Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 38 Works and Transport Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 496 2023-06-01

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga daraja linalounganisha Kata ya Bokwa na Songe Kilindi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Kilindi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kazi ya ujenzi wa Daraja la Songe katika barabara ya Kwaluguru – Kiberashi linalounganisha Kata ya Bokwa na Songe na barabara zake unganishi imekamilika tarehe 30 Novemba, 2022. Kwa sasa mkataba upo katika kipindi cha uangalizi hadi tarehe 29 Novemba, 2023, ahsante.