Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 38 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 492 2023-06-01

Name

Stanslaus Shing'oma Mabula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA K.n.y. MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza: -

Je, Serikali haioni kutoa fedha za ujenzi wa vituo vya afya kwa kigezo cha idadi ya tarafa ni kuwanyima wananchi vituo vya afya?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI): alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Shing’oma Mabula, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kati ya tarafa 570 zilizopo 211 hazikuwa na kituo cha afya hata kimoja, hivyo Serikali ilitoa kipaumbele cha ujenzi wa vituo vya afya kwenye tarafa ambazo hazina kituo cha afya. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali ilijenga vituo vya afya 234. Kipaumbele cha ujenzi kilizingatia tarafa ambazo kata zake hazikua na kituo cha afya. Aidha, ujenzi wa kituo cha afya ulizingatia kata za kimkakati.