Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 35 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 454 2023-05-29

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza: -

Je, ni lini ahadi ya kujenga Kituo cha Afya Kata ya Kasanga itatekelezwa?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI): alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kasanga kama iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivyotembelea Kata ya Kasanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati kote nchini kikiwemo Kituo cha Afya Kasanga kama ilivyoelekezwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu.