Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 29 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 371 2023-05-19

Name

Ally Juma Makoa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kondoa Mjini

Primary Question

MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule ya Bweni ya Wasichana katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Juma Makoa, Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Mji wa Kondoa tayari ina shule moja ya wasichana ya Serikali inayoitwa Kondoa Girls. Shule hii ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 660. Kwa sasa shule ina wanafunzi 572 wa kidato cha tano na sita na Halmashauri imeomba kuongezewa mchepuo wa HGE ili iweze kutumika kwa full capacity.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuongeza shule za bweni za wasichana kulingana na uhitaji na upatikanaji wa fedha.