Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 33 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 429 2023-05-25

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaongeza majengo katika Kituo cha Afya cha Matamba Wilayani Makete?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makete, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2022 Serikali ilitenga na kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya vinne vya Ipelele, Kitulo, Bulongwa na Lupalilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa vituo vya afya kwenye maeneo ya kimkakati ikiwemo kuongeza majengo ya Kituo cha Afya Matamba katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete kadri ya fedha zitakavyopatikana.