Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 26 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 337 2023-05-16

Name

Kassim Hassan Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanakwerekwe

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. KASSIM HASSAN HAJI aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kubadili utaratibu wa malipo kwa wastaafu wa Jeshi la Polisi wa Zanzibar ili kuondoa usumbufu wanaoupata?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimwa Kassim Hassan Haji, Mbunge wa Mwanakwerekwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali utumishi wa Askari Polisi ulikuwa kwenye masharti ya pensheni na bakshishi. Askari ambaye hakuwepo kwenye masharti ya pensheni alifanya kazi kwa mkataba wa miaka 12 kwa kujaza mkataba wa kipindi cha kila baada ya miaka mitatu kumalizika. Kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322, askari kwa hiari yake mwenyewe baada ya mkataba alipaswa kufanya chaguo la ama kuendelea na utaratibu wa ajira ya mkataba na kwa malipo ya bakshishi ambao ukomo wake wa utumishi ni miaka 21 au kuingia kwenye utaratibu wa ajira ya malipo ya pensheni na kulipwa mafao ya uzeeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni Jeshi la Polisi limefanya maboresho kwa kuondoa utaratibu wa mkataba wa miaka 12 na kuwa miaka sita pamoja na kuondoa chaguo. Na baada ya mkataba kumalizika askari wote wanaingia kwenye ajira ya kudumu yaani pensheni.