Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 23 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 296 2023-05-11

Name

Hassan Seleman Mtenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Daraja la Kilambo?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hasan Seleman Mtenga, Mbunge wa Mtwara Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Daraja la Kilambo linalopendekezwa kujenga litaunganisha Nchi ya Tanzania na Msumbiji katika Barabara ya Mangamba – Madimba – Tangazo – Kilambo yenye kilometa 36.8 Mkoani Mtwara. Kwa kuwa ujenzi wa daraja hili utahusisha Nchi mbili za Tanzania na Msumbiji, Serikali tayari imeanza mazungumzo ya awali na Nchi ya Msumbiji ili ziweze kukubaliana kuhusu ujenzi wa daraja hilo, ahsante.