Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 23 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 292 2023-05-11

Name

John Michael Sallu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Vijijini

Primary Question

MHE. JOHN M. SALLU aliuliza: -

Je, ni lini Kituo cha Afya katika Kata ya Segera, Tarafa ya Mkumbulu kitajengwa?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA YA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa John Marko Sallu, Mbunge wa Handeni Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali ilitenga fedha shilingi bilioni 117 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati katika kata 234 kote nchini. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ilipewa shilingi milioni 500 ya ujenzi wa Kituo cha Afya Sindeni.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya kwenye Kata za kimkakati nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya Segera katika Tarafa ya Mkumbulu.