Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 22 Works, Transport and Communication Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 289 2023-05-10

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FROLENT L. KYOMBO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaongeza minara au kuboresha mawasiliano katika kata zote 20 za Wilaya ya Misenyi?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA NA HABARI, alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Frolent Laurent Kyombo Mbunge wa Nkenge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imetekeleza miradi ya mawasiliano iliyokamilika katika kata 10 za Wilaya ya Missenyi. Kufikia mwezi Machi, 2023 tayari ujenzi wa minara 13 imekamilika na inatoa huduma katika teknolojia ya 2G na 3G.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali Serikali imeshapata watoa huduma wa kufikisha huduma za mawasilioano katika Kata za Bugorora, Kasambya, Mutukula na Kakunyu ambapo tayari zimeshapata watoa huduma, ahsante.