Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 22 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 288 2023-05-10

Name

Taska Restituta Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mpanda hadi Karema kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Taska Restituta Mbogo, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) tayari imekamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya kilometa 10 ya kutoka Mpanda hadi Kagwira na kwa sehemu iliyobaki ya kuanzia Kagwira hadi Karema (kilometa 112) zabuni za kuwapata Makandarasi zilitangazwa tarehe 20 Aprili, 2023 na zimepangwa kufunguliwa tarehe 31 Mei, 2023, ahsante.