Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 22 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 286 2023-05-10

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI K.n.y. MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Rungwe?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niamba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, taratibu za ajira zinaendelea kuchakatwa ili kupata Wenyeviti 57 watakaoweza kukamilisha uhitaji wa Wenyeviti 139 ambayo ni idadi ya Wilaya zote hapa nchini. Kwa sasa tuna Wenyeviti 82 tu ambao wanalazimika kuhudumia Wilaya zisizo na Mabaraza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Wilaya ya Rungwe inahudumiwa na Mwenyekiti kutoka Wilaya ya Kyela.