Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 22 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 283 2023-05-10

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Mahakama yenye hadhi ya Wilaya katika Wilaya ya Kalambo?

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepanga kuanza ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Kalambo katika mwaka huu wa fedha 2023/2024 ambapo taratibu zote za awali za kupitia michoro na makadirio ya gharama vimekamilika. Aidha, hatua ya kupata Mkandarasi wa ujenzi ipo katika hatua za mwisho. Hivyo, tunategemea muda wowote jengo hili litaanza kujengwa na kukamilika katika mwaka ujao wa fedha, ahsante.