Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 16 Works, Transport and Communication Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 203 2023-05-02

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: -

Je, ni lini umeme utafungwa kwenye mnara wa halotel uliopo kata ya Ngujini Wilayani Mwanga?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zuena Athumani Bushiri Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Jukumu la kuunganisha umeme kwenye minara ya mawasiliano ya simu nchini, ikiwemo ile iliyojengwa kwa ruzuku ya Serikali, ni jukumu la watoa Huduma, hii ni pamoja na gharama za kuunganisha umeme na kuendesha minara husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kusimamia huduma za mawasiliano nchini kwa kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi matakwa ya leseni zinazotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).