Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 16 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 201 2023-05-02

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kurudia ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi – Maswa ambayo imejengwa chini ya kiwango na imeshaharibika?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Lukago Midimu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mkandarasi alianza kazi za kurudia ujenzi wa maeneo yote ambayo yalionekana hayakidhi viwango vya ujenzi kwa gharama zake mwenyewe mnamo tarehe 10 Juni, 2021. Kazi za marudio ziko katika hatua za mwisho ambapo zimefikia asilimia 98 na zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei, 2023.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.