Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 16 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 198 2023-05-02

Name

Kiswaga Boniventura Destery

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Magu

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali italipa kiinua mgongo kwa wazee ambao hawajawahi kuajiriwa?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kiinua mgongo ni malipo ambayo hulipwa na mwajiri pindi mfanyakazi wake anapostaafu kufanya kazi. Hata hivyo, kutokana na kuwepo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambapo mwajiriwa na mwajiri huchangia, mfanyakazi hulipwa pensheni badala ya kiinua mgongo na hupokea mafao ya mkupuo mara anapostaafu na badaye kuendelea kulipwa pensheni ya kila mwezi kwa maisha yake yote. Hivyo, kwa sasa hakuna mfumo wa kulipa kiinua mgongo kwa mzee ambaye hajawahi kuajiriwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.