Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 13 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 174 2023-04-25

Name

Maulid Saleh Ali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Welezo

Primary Question

MHE. MAULID SALEH ALI aliuliza: -

Je, kuna mkakati gani wa kudhibiti utapeli unaofanywa kwa kutumia namba za simu za nje?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maulid Saleh Ali, Mbunge wa Jimbo la Welezo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, utapeli ama kwa lugha nyingine ni udanganyifu unaofanywa kwa kutumia simu za nje hudhibitiwa kwa kushirikisha Mamlaka za Udhibiti kwenye nchi ambako namba zinazotumika zimegawiwa. Mamlaka hizo huchukua hatua stahiki kwa kadri wanavyopokea taarifa zinazohusiana na utapeli huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ni Mwanachama wa Jumuiya za Kikanda na Kimataifa kama vile ATU, EACO, CRASA, CTO, ITU, UPU, PAPU na kadhalika. Ushirikiano uliopo kupitia Jumuiya hizi husaidia sana kwenye utatuzi wa masuala mengi yakiwemo yanayohusu utapeli unaofanyika kwenye mitandao ya simu.