Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 13 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 170 2023-04-25

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA (K.n.y. MHE. HAWA S. MWAIFUNGA) aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwalinda watoto walio tayari kwenye ndoa wakiwa na umri mdogo?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshmiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Mwaifunga, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, wasichana walioolewa pia wameunganishwa na fursa za kujiunga na vyuo na kupata mafunzo ya muda mfupi katika fani mbalimbali kupitia vyuo vya ufundi VETA na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na Ustawi wa Jamii ambavyo vipo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Mafunzo watakayopata yanaweza kuwasaidia kujiajiri au kuajiriwa katika ya Sekta ya Umma na Binafsi.

Aidha, Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imekuwa ikiendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana kwenye fani mbalimbali za uwanagenzi zikiwemo shughuli za kilimo cha mazao ya muda mfupi, ufugaji, uhunzi wa vifaa na bidhaa, ususi, uchoraji, ushonaji, pamoja na shughuli nyingine sawa na mahitaji yatakayoibuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutekeleza miradi hii kwa lengo la kumwinua na kumwezesha mtoto wa kike ili aweze kuwa huru na kujitegemea, ahsante.