Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 13 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 160 2023-04-25

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: -

Je, ni lini Kituo cha Afya Bukene kitapatiwa mashine ya x- ray na ultrasound?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Seleman Jumanne Zedi, Mbunge wa Jimbo la Bukene, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya Bukene kinatoa huduma za kiuchunguzi ambapo kwa sasa kina mashine ya Ultrasound. Aidha, kituo hiki hakina miundombinu ya jengo la kuwezesha utolewaji wa huduma za X-Ray. Serikali itaendela kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya afya pamoja na ununuzi wa mashine za uchunguzi ikiwemo X-Ray na Ultrasound kwa ajili ya vituo vya huduma nchini ikiwemo Kituo cha Afya cha Bukene, ahsante.