Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 54 2022-04-13

Name

Tabasamu Hamisi Hussein Mwagao

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sengerema

Primary Question

MHE. TABASAM H. MWAGAO aliuliza: -

Je, ni lini miradi ya umwagiliaji katika Vijiji vya Nyamterela na Katunguru pamoja na Vijiji vya Kwinda na Isole itakamilika Wilayani Sengerema?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tabasam Hamis Mwagao, Mbunge wa Sengerema, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/ 2023, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bwawa na miundombinu ya umwagiliaji katika skimu ya Katunguru yenye hekta 600 iliyopo kijiji cha Nyamterela Wilayani Sengerema.

Vilevile Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa bwawa na miundombinu ya umwagiliaji katika skimu ya Usole yenye hekta 1,000 iliyopo katika kijiji cha Kishinda.