Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 136 2022-09-23

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Primary Question

MHE. DANIEL B. SILLO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Gidas?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sillo Daniel Baran, Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua uhitaji mkubwa uliopo wa magari ya kubebea wagonjwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19 imefanya manunuzi ya magari 195 ya kubebea wagonjwa ambayo yatapelekwa kwenye Halmashauri zote nchini ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Babati.