Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 7 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 100 2023-11-07

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka huduma ya mawasiliano ya simu Kata ya Masaka – Kalenga?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jackson Gedion Kiswaga, Mbunge wa Jimbo la Kalenga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) iliingiza Kata ya Masaka katika zabuni ya kufika huduma ya mawasiliano Vijijini kupitia Mradi wa Tanzania ya Kiditali, ambapo Kampuni ya Simu ya Vodacom ilishinda zabuni hiyo ya kufikisha huduma hiyo katika Kata ya Masaka yenye Vijiji vya Kaning’ombe, Saadani pamoja na Makota. Mpaka sasa Vodacom inaendelea na hatua mbalimbali za utekelezaji katika ujenzi wa mnara huo.