Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asya Mwadini Mohammed

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASYA MWADINI MOHAMED K.n.y. MHE. KAPT. ABBAS ALI MWINYI aliuliza:- Je, ni kero gani za Muungano bado hazijapata ufumbuzi hadi sasa; na ni jitihada gani zinafanyika ili kero zilizosalia zipate ufumbuzi?

Supplementary Question 1

MHE. ASYA MWADINI MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Nina swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa, kuna kero Saba ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi na kuna kero nyingine ambazo wameanza kuzipatia ufumbuzi. Je, ni nini mpango wa Serikali kuhusiana na utoaji wa taarifa wa kero hizi ili wananchi waweze kujua tathmini na ufuatiliaji wa kero ngapi ambazo zimetatuliwa na ngapi ambazo hazijatatuliwa kwa maslahi mapana ya Taifa? Ahsante.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali zuri la Dada yangu, Mheshimiwa Asya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli safari yetu ya utatuzi wa hoja za muungano kama mnavyokumbuka tulikuwa na hoja 25, katika hoja hizo mwaka 2010 tulitatua hoja Mbili, mwaka 2020 tukatatua hoja Tano. Katika kipindi hichi cha mwaka mmoja chini ya Kiongozi Mama Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi tulitatua hoja 11. Kwa hiyo, tumefanikisha kumaliza kutatua hoja 18 za Muungano kati ya hoja 25, kwa hiyo tumebakiwa na hoja Saba. Utaratibu wetu ni kwamba tarehe 23 Agosti, 2021 jambo kubwa lililofanyika Zanzibar ilikuwa ni kuitisha vyombo vya habari na kuwaeleza wananchi kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo tumejipanga kupitia vikao mbalimbali ndiyo maana katika bajeti tuliyopitisha mwaka huu tumetoa maelekezo ya kina na kutenga bajeti maalum ya kutoa elimu ya upana kwa suala la muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo jambo hili linaendelea kuwapa wananchi katika taarifa mbalimbali kupitia runinga, vyombo vya habari mbalimbali, magazeti hali kadhalika redio zetu ikiwa ni pamoja na zile local radio zetu.

Name

Najma Murtaza Giga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASYA MWADINI MOHAMED K.n.y. MHE. KAPT. ABBAS ALI MWINYI aliuliza:- Je, ni kero gani za Muungano bado hazijapata ufumbuzi hadi sasa; na ni jitihada gani zinafanyika ili kero zilizosalia zipate ufumbuzi?

Supplementary Question 2

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa tafsiri ya kamusi ya Kiswahili – English, kero maana yake ni a noise, a noise ni kama maudhi ambayo ndiyo hizo kero zenyewe. Maudhi yakiendelea hata kwenye ndoa inaweza kusambaratika. Je, Serikali haioni umuhimu wa kubadilisha hili neno na kuweka japo changamoto tukizingatia kwamba hizi changamoto ni endelevu kila siku zinakuja na zingine zinaondoka?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Dada yangu, Mheshimiwa Najma Giga, ambaye ni Mbunge machachari sana na Mwenyekiti wetu wa Kamati ya Bunge hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli ushauri wake ni mzuri na ndiyo maana sasa hivi tunavyopeleka taarifa sasa hivi tunaita ni hoja za Muungano siyo kero za Muungano. Kwa vile mafanikio ni makubwa zaidi kulikoni hizi hoja, kwa hiyo jambo hili Mheshimiwa Mbunge tumelichukua na tunaendelea kulifanyia kazi na hakika ninawaomba Watanzania kwa ujumla, sasa tuendelee kuhubiri zaidi mafanikio zaidi katika utekelezaji wa mambo Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.