Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. AIDA J. KHENANI K.n.y MHE. AGNESTA L. KAIZA aliuliza:- Je, kwa nini Serikali isisamehe kodi na kuondoa baadhi ya tozo katika Sekta ya Elimu na Afya ili kuvutia taasisi binafsi?

Supplementary Question 1

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, natambua msamaha ambao umetajwa na Serikali, lakini pamoja na msamaha unaotolewa wa kodi unakuwa sawa kwenye hizi taasisi lakini wanapotoa hizi huduma, wanatoa kwa gharama tofauti tofauti. Serikali ipo tayari kutoa mwongozo sasa katika hizi gharama zinazotelewa kwenye hizi taasisi binafsi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, pamoja na misamaha ya Kodi ya Ongezeko la Thamani bado kuna changamoto ya Kodi ya Forodha kwa vifaa tiba pamoja na dawa.

Je, Serikali iko tayari kutoa hizi kodi zote kama ilivyotangaza kwenye magari yanayotumia umeme ili kutoa kipaumbele kwa afya za Watanzania? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Aida kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa taasisi ambazo zinafanya biashara zinastahiki kutoa kodi inayostahiki kwa mujibu wa sheria, ambazo zinatoa huduma tu zinapata hadhi ya charitable organization na zitapata unafuu wa kodi.

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili, Serikali inatambua umuhimu uliopo katika elimu na afya, tunaendelea kuboresha miongozo mbalimbali ya kodi ili kila wakati tuweze kufikia malengo ya utoaji huduma bora kwa wananchi wetu, ahsante.