Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Salma Rashid Kikwete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mchinga

Primary Question

MHE. SALMA R. KIKWETE K.n.y. MHE. JUDITH S. KAPINGA aliuliza:- Je, Serikali inafanya nini kuhakikisha uviaji mimba usio salama unakwisha?

Supplementary Question 1

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu ya Serikali. Nina swali la nyongeza. Kwa kuwa utoaji wa Mimba siyo kitu kizuri na kinahatarisha maisha ya wasichana: Je, elimu hiyo ambayo mmeitoa, imetolewa kwa kiwango gani au katika mikoa mingapi ya nchi yetu ya Tanzania? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba elimu ni mchakato endelevu na ni mchakato ambao watoto wanapata mashuleni, lakini kila akina mama wanapohudhuria kliniki tunawapa elimu na vile vile, kuna vipindi mbalimbali vinavyotolewa kwenye tv ambavyo vinawafikia wananchi. Kwa hiyo, kimsingi hakuna Mkoa wala wilaya ambayo elimu hiyo haijatolewa.