Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Venance Methusalah Mwamoto

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. VENANCE M. MWAMOTO (K.n.y. MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE) aliuliza:- Katika Jimbo la Muhambwe kuna Chuo cha Wauguzi (MCH) ambacho ni muhimu sana katika sekta ya afya, lakini hakiko katika hali nzuri. Je, Serikali ina mpango gani wa kukiboresha chuo hicho na vingine vya aina hiyo ili viweze kujiendesha na kulipa wazabuni wengi ambao wanawadai?

Supplementary Question 1

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa Wilaya ya Kibondo ni Wilaya ambayo ilikaliwa na wakimbizi na kwa kuwa kuna majengo ambayo yamekaa kwa muda mrefu ya IOM ambayo Serikali ya Wilaya na Mkoa ilisharidhia kwamba yatumike kwa ajili ya chuo hicho. Je, Waziri haoni sasa ili kubana matumizi ya Serikali afike na kutoa ushauri ili yale majengo yatumike kwa ajili hiyo?
Mheshimiwa Mwenyekiti swali la pili, kwa kuwa makampuni mengi ya ujenzi baada ya kujenga barabara yamekuwa yakiacha miundombinu ya majengo mazuri. Sasa haoni ni wakati muafaka wa kupunguza upungufu wa wauguzi zikiwepo Wilaya nyingi pamoja na Kilolo kwa kuweza kuyatumia yale majengo vizuri ili Serikali iweze kupata manufaa?

Name

Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwamba nifike Kibondo ili nikashauriane na Serikali ya Mkoa ambao wameshapitisha azimio la kutaka kutumia majengo yaliyoachwa na IOM namwahidi nitafika mara baada ya Bunge la Bajeti kukamilika ili nishirikiane na Serikali ya Mkoa nione kwa ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo wana dhamana ya mali na maeneo yote ya wakimbizi, ni nini Serikali itafanya ili kuwezesha azimio lao hilo mkoani kutekelezeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuhusiana na majengo yaliyoachwa na miradi mbalimbali ya ujenzi; taratibu kwa kweli zimekuwa ni hivyo kama anavyopendekeza Mheshimiwa Mbunge. Hivyo, wafuate taratibu za kuzungumza ndani ya vikao vyao vya kufanya maamuzi kwenye halmashauri husika, ili walete mapendekezo Serikali Kuu tuone kama yanaweza yakapitishwa na wanaohusika na mradi huo kutumika kwa ajili ya shughuli ambazo wanazipendekeza.