Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza:- Je, kwa kodi ya mapato kwa wachimbaji wadogo wa madini isiunganishwe na Mineral Market Management Information System (MMMIS)?

Supplementary Question 1

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Mkoa wa Iringa una potential kubwa ya madini ya chuma pamoja na madini ya viwandani, je, Wizara ya Fedha iko tayari kutuunganisha na wadau ili tuweze kutumia potential hiyo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Mkoa wa Iringa pia umekuwa ukikusanya maduhuli kila mwaka takribani bilioni moja kutokana na madini. Sasa Wizara ya Fedha ipo tayari kuwa na mpango mahususi kuisaidia GST na STAMICO kufanya utafiti wa kijiolojia ili tuongeze mapato hayo na yenyewe inufaike? (Makofi)

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la kwanza, Wizara ya Fedha tuko tayari na Mheshimiwa Mbunge kabla ya kurudi Jimboni tufanye kikao ili tuweze kumuunganisha na Idara inayosimamia hiyo ili aweze kuwaunganisha na wadau aliowataja kwa ajili ya kufanikisha hilo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu lile la pili, GST pamoja na taasisi zingine kuhusu kuongeza utafiti zaidi, tulishaongea na Wizara ya Kisekta na tuko tayari kuongeza fedha ili utafiti zaidi uweze kufanyika, kwa sababu potential ya kugundua maeneo mengine ya uchimbaji bado ipo na inaweza ikatuletea tija zaidi. (Makofi)