Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwantakaje Haji Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Bububu

Primary Question

MHE. MWANTAKAJE HAJI JUMA aliuliza:- Je, lini Kituo cha Polisi Bububu pamoja na nyumba za Askari vitafanyiwa ukarabati?

Supplementary Question 1

MHE. MWANTAKAJE HAJI JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Nilikuwa na swali moja, hiki kituo ni chakavu na cha miaka mingi, miundombinu yake ni mibovu; je, Naibu Waziri yuko tayari kuongozana nami kwenda kujionea kituo hicho? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ama Wizara ya Mambo ya Ndani tupo tayari kuja kukagua na kuona uchakavu wa kituo hicho ili kuona namna ya kuweza kupata hizi fedha na kuanza kukifanyia ukarabati, nakushukuru.