Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Anania Tadayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatekeleza mradi wa kuondoa magugu maji katika Ziwa Jipe?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninapenda kuuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo hilo la magugu maji katika Ziwa Jipe limedumu zaidi ya miaka 20 sasa, na imekuwa ni ahadi ya Serikali kila wakati ya kuondoa magugu maji hayo. Pamoja na shukrani kwa Mheshimiwa Rais kupitia kwa Mheshimiwa Waziri alimtuma Naibu Waziri akaja kuwapa ahadi hiyo wananchi, lakini Serikali haioni sasa kwamba umefika wakati kwa vile tatizo hili limekuwa kwa muda mrefu sana, ziko mashine hizi aquatic wild harvesters nyingi sana China na kila mahali ambazo thamani yake haizidi hata dola laki tano, ambazo zinaweza zikafanya kazi hii kwa namna endelevu kidogo kidogo ili kuzuia kuendelea kwa uharibifu wa mazingira na pia kuwawezesha wananchi wa Mwanga kuendelea kufaidi matunda ya lile Ziwa wakati Serikali inaendelea na mpango mkubwa huo wa mabilioni ya fedha ambao tunausubiri kwa hamu, ahsante.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la kaka yangu Mheshimiwa Joseph Tadayo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninapenda kushukuru sana Mheshimiwa Mbunge amekuwa akielezea hoja hii mara nyingi sana na ndiyo maana takribani wiki nne zilizopita nilimtuma Naibu wangu, Mheshimiwa Chilo alienda kule kwa ajili ya kuangalia uhalisia ulivyo. Kama nilivyosema ni kwamba tunaendelea na mchakato huu na andiko letu hili ni kwa ajili ya Ziwa Jipe na hali kadhalika Ziwa Chala lakini maoni ya Mheshimiwa Mbunge naomba niseme kwamba Ofisi yetu imeyachukuwa, lengo letu ni kwamba kuhakikisha tunatumia mbinu zote zinazowezekana, hili itaangalia fursa zote zinazopatikana hata tukipata mradi kidogo wa muda mfupi, nini kifanyike lakini jambo kubwa la pale litaendelea kufanyika katika mradi huu lakini lile wazo la kwanza lakini wazo lako tunalichukua kwa ajili ya kulifanyia kazi Mheshimiwa Mbunge.

Name

Vedastus Mathayo Manyinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Musoma Mjini

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatekeleza mradi wa kuondoa magugu maji katika Ziwa Jipe?

Supplementary Question 2

MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ziwa Victoria mwaka jana lilichafuka sana na likasababisha Samaki wengi wakafa hasa wale watu waliokuwa wametengeneza Vizimba wakapata hasara kubwa, Serikali ilipotuma wataalam waliweza kusema kwamba ni kwa sababu ya vinyesi vya mifugo kwa maana ya ng’ombe ndiyo vimesababisha hali hiyo imetokea, yale majibu hakuna yeyote aliyekubaliana nayo.

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba hali hiyo haijitokezi tena ili wananchi wanaoishi Kanda ya Ziwa wasiendelee kupata hasara?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mathayo, Mbunge wa Musoma kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tulipata changamoto sana katika Ziwa Victoria, changamoto hii ilisababishwa na suala zima la mkondo wa Mto Mara ulikuwa unashuka kule, hili kama tulivyosema ni kwamba lengo letu ni kwamba hatuhitaji wananchi waweze kupata hasara na katika hili ndiyo maana msisitizo wetu mkubwa ulikuwa ni jinsi gani wananchi kupewa elimu ya utunzaji wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maeneno mbalimbali tulivyoona miongoni mwa changamoto kubwa inayotokea ni uhalibifu wa mazingira. Leo hii hatuzungumzii Ziwa Victoria peke yake hata Ziwa Babati hivi karibuni, unaona kwamba ongezeko la magugu maji. Ndiyo maana Ofisi ya Makamu Wa Rais, Muungano na Mazingira ilichokifanya ni nini hivi sasa? Ilichokifanya sasa hivi ni kuandika maandiko mengi kwa pamoja na siyo linalozungumzia suala la Ziwa Jipe peke yake lakini sasa hivi tuna suala zima la Ziwa Babati, na eneo lote la Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jukumu letu ni kuona jinsi gani tutafanya tupate mbinu mbadala ya kuhakikisha maeneo haya yote tunayatunza kwa lengo la kuwasaidia wananchi na uchumi wao. Ahsante sana.