Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza: - Je, watalii wangapi walitembelea Mbuga ya Ruaha kwa mwaka 2019/2020 na upi mkakati wa kuongeza watalii?

Supplementary Question 1

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika Awamu ya Tano ambayo kupitia RIGRO walipendekeza kwamba lengo kubwa ni kukuza utalii Kusini na walichagua Mkoa wa Iringa uwe ni makao makuu ya mradi huo. Sasa tumeshatenga eneo lipo na kila mwaka tunaadhimisha wiki ya utalii pale Mkoa wa Iringa.

Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha utekelezaji wa makao makuu haya unafanyika? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba wananchi walioko pembezoni mwa mbuga hii wanapata elimu, wanawezeshwa kielimu na kiuchumi kuhakikisha kwamba wao ndio watakaokuwa watangazaji wa mbuga hii?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwanza niendelee kuwapongeza Wabunge wote wa Iringa, pamoja na kuwa swali hili na Mheshimiwa Grace Tendega, lakini mara nyingi wanafuatilia sana kwenye mradi huu wa RIGRO na ujenzi wa information center ambayo itajengwa Makao Makuu Iringa uko kwenye hatua za kuanza. Tayari tulikuwa kwenye mkakati wa mkandarasi ambaye tayari tulikuwa tumeshatangaza kazi na tuko anytime kuanza kazi hii. Kwa hiyo, naomba niwataarifu tu kwamba Wana-Iringa na Watanzania wote kwa ujumla kwamba utalii na mkakati wa kukuza utalii Kusini mwa Tanzania uko mbioni kuanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala hili la kuwapa elimu wananchi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi; kwenye Mradi wa RIGRO zimetengwa fedha kwa ajili ya kuwapeleka training wananchi mbalimbali waliozunguka katika maeneo yanayozunguka mradi huu, na ni shahidi tosha Wabunge wanaotoka katika maeeo hayo wanafahamu kwamba tumekuwa tukipeleka watoto ambao wanapelekwa shuleni kwa ajili ya kujifunza namna ya kuendeleza masuala mazima ya utalii na uhifadhi. Kwa hiyo, faida wameshaanza kuziona na wananchi wameshaanza kuona faida ya mradi huu.

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza: - Je, watalii wangapi walitembelea Mbuga ya Ruaha kwa mwaka 2019/2020 na upi mkakati wa kuongeza watalii?

Supplementary Question 2

MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya changamoto kubwa kwenye sekta hii ya utalii ni uhaba wa hoteli zenye hadhi ya kulaza wageni wetu; je, Serikali ina mkakati gani wa kutatua changamoto hii?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa sasa tayari Serikali imeshaanza kutangaza maeneo ya uwekezaji na tayari wawekezaji wameshaanza kujitokeza. Kwa hiyo, suala la uhaba linaenda kupungua ama kuisha kabisa kutokana na uzinduaji wa filamu ya Royal Tour na mkakati wa uwekezaji ambao tayari tumeshaanza kuuweka.

Name

Jeremiah Mrimi Amsabi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza: - Je, watalii wangapi walitembelea Mbuga ya Ruaha kwa mwaka 2019/2020 na upi mkakati wa kuongeza watalii?

Supplementary Question 3

MHE. JEREMIAH M. AMSABI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa ajili ya kuongeza idadi ya watalii na kuboresha uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti; je, ni lini ujenzi wa uwanja wa ndege wa Serengeti utaanza?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba tu niwataarifu ndugu zangu wana-Serengeti, hususan Mugumu kwamba mchakato unaendelea na uko kwenye hatua za utekelezaji kwa maana ya kuanza. Tayari tulishaanza mchakato na namna ya ku-identify hayo maeneo na lengo ni kuhakikisha kwamba tunapunguza muingiliano wa shughuli za uhifadhi katika Hifadhi ya Serengeti, hivyo uwanja tutauhamisha usogee katika Eneo la Mugumu. Kwa hiyo, mchakato unaendelea.

Name

Dennis Lazaro Londo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mikumi

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza: - Je, watalii wangapi walitembelea Mbuga ya Ruaha kwa mwaka 2019/2020 na upi mkakati wa kuongeza watalii?

Supplementary Question 4

MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya jitihada za kuongeza watalii dunia nzima ni kurahisisha miundombinu, hasa barabara na mageti kutokea kila upande. Kuna maelekezo ya Serikali pale Mbuga ya Mikumi kufungua geti lingine kwa upande wa Kilangali na Tindiga ili kurahisisha usafiri wa watalii kutokea Kilosa kwenye station ya SGR itakapokamilika.

Je, Serikali ina kauli gani? Lini geti hili linaenda kufunguliwa kuheshimu maelekezo ya Makamu wa Rais, lakini wewe pia Naibu Waziri ulipoitembelea Mikumi?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, tunatambua kwamba, geti hili ni la muhimu sana kwa ajili ya uchumi wa nchi, hususan katika masuala mazima ya utalii na tayari tulishaanza mpango wake. Kwa hiyo, nimuondoe shaka Mheshimiwa Mbunge wa Mikumi kwamba geti hili tutalifungua na pale tu ambapo mchakato wa reli utakavyoanza tayari na sisi utekelezaji wake utakuwa umekamilika.