Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kutatua changamoto za wakulima waliowekeza kwenye SACCOS na fedha zao kupotea?

Supplementary Question 1

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tatizo hili katika Jimbo la Moshi Vijijini limekuwa kubwa sana; je, Naibu Waziri upo tayari kuambatana na Profesa Ndakidemi kwenda kutatua changamoto hiyo?

Swali la pili, katika Jimbo la Hai SACCOS ya Kware, SACCOS ya Lyamungo, Masama Mula, Mudio na Lemira, wananchi walihamasishwa kujiunga na SACCOS hizi baadae viongozi wale walitoroka na fedha za wanachama.

Je, ni lini Serikali itakwenda katika Wilaya ya Hai kutatua changamoto hizi ikiwa ni Pamoja na kurudisha fedha za wanachama wa SACCOS nilizozitaja? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la kwanza nipo tayari kuongozana na Mheshimiwa Mbunge kwenda katika Jimbo lake kuangalia changamoto zilizopo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, natumia fursa hii kumuelekeza Mrajisi wa Vyama vya Ushirika kuhakikisha kwamba anatuma timu yake kwenda kufanya uchunguzi wa awali juu ya jambo hili na baadaye hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wale wote ambao wametoweka na fedha za wanachama.