Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza: - Je, lini Daraja la Lyusa na Itembe na kalavati la Nkoma, Lyusa na Mwanjolo vitajengwa ili Daraja la Sibiti lipitike mwaka mzima?

Supplementary Question 1

MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Majibu aliyoyatoa yako sahihi na kama yatatekelezeka, Meatu tutafaidika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mpango huu wa kujenga madaraja haya kwa kupitia barabara hiyo ya lami itakuwa ni mwezi Oktoba: Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kujenga madaraja haya kwa muda mfupi, Lyusa pamoja na Chobe ili wananchi wa Meatu waendelee kutumia ile barabara kwa mwaka mzima? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Minza yote kwa pamoja, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi, haya madaraja ni madaraja aina ya drift, na katika mpango ambao tutaujenga sasa kwa mpango mkubwa wa EPC+F, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi, tunategemea mradi huu usainiwe kabla ya mwisho wa mwezi Juni. Kwa hiyo, tumejumuisha hayo madaraja, yatajengwa wakati huo mradi mkubwa unatekelezwa, ahsante. (Makofi)