Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kudhibiti magari yanayopakua na kupakia mizigo katika maeneo ya Kariakoo, Mtaa wa Msimbazi na Barabara ya Morogoro ili kupunguza kero kwa wakazi wa maeneo hayo?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Pamoja na vibali na eneo lililotengwa, lakini bado kadhia ya magari makubwa hupaki, kupakua na kupakia mizigo katika Barabara kama za Nyati, Faru, Tembo na kadhalika inaendelea.

Je, Serikali inaelewa kwamba wafanyabiashara hawa wa mizigo wanawakosesha haki ya kimsingi wanye makazi ya kulala, pia kuharibu utaratibu mzima wa afya ya akili?

Je, ukitokea moto, wakati barabara zote zimezibwa na magari makubwa haya ya mizigo, Serikali haioni kama hilo janga in the make, ina mpango gani?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Asha Abdullah Juma, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, cha kwanza tunatambua haki za msingi za wananchi wa maeneo hayo wanayokaa na kero wanayoipata. Kwa hiyo, kutokana na umuhimu wake, sisi kama ofisi ya Rais TAMISEMI, tunaomba tulipokee na tuangalie namna bora ambayo tunaweza tukaifanya kuchukua hatua za haraka.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili la msingi, kuhusu majanga ya moto, tumesema moja ya mkakati wetu na mkakati wa Jiji la Dar es Salaam ni kujenga eneo jipya katika eneo la Mnazi Mmoja kwaajili ya maegesho ya magari. Kwa hiyo, kwa kuuliza hili swali la msingi maana yake sasa tutaiharakisha Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ianze huo mkakati hara iwezekavyo ili muondokane na hiyo kero. Ahsante.

Mheshimiwa Naibu Waziri tunakushukuru sana kwa majibu yako kwa maswali ya Waheshimiwa Wabunge. Wizara ya Maji, Mheshimiwa Jafari Wambura Chege, Mbunge wa Rorya sasa ulize swali lake.