Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kurasimisha, kupanga na kupima ardhi katika Miji Midogo ya Mawengi, Lugarawa, Luilo na Manda – Ludewa?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, ila napenda kufahamu kwamba: Je, Mheshimiwa Waziri haoni sasa ni muda muafaka wa kufanya ziara Ludewa kwenda kutembelea hizo kazi na kugawa hati zile za mwanzo kwa wananchi ili kuongeza hamasa? Ahsante. (Makofi)

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kamonga, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kumhakikishia Mbunge kwamba umuhimu huo tunauona ndani ya Wizara na niko tayari sasa kuongozana naye baada ya Bunge kwenda kukabidhi ardhi zilizogaiwa ili kutengeneza hamasa kwa wengine waweze kujitokeza kwa wingi.