Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maimuna Ahmad Pathan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaunda tena Bodi ya Wataalam wa Ugavi na Ununuzi (PSPTB) baada ya kuvunjwa kwa muda mrefu?

Supplementary Question 1

MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa jibu zuri ambalo nimelipata: -

Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati upi ambao imeuweka wakati mwingine isijirudie kukaa muda mrefu bodi za wataalam kutokuwepo?

Mheshimiwa Spika, Ahsante.

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Maimuna Ahmad Pathan, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imejiandaa na imeweka mipango, mikakati na taratibu maalum ambazo zitakuwa ni suluhisho sahihi la kutokuwa na muda mrefu wa kuunda ama kuteuwa bodi hizo. Ahsante.