Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dorothy George Kilave

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je ni lini Serikali itamaliza mgogoro wa Ardhi kati ya Wananchi na Serikali katika Kata ya Yombo Vituka?

Supplementary Question 1

MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Ili kuepusha hii migogoro: Je, ni lini sasa Serikali itaweza kwenda kuweka mipaka halisi ya ile sehemu ili tuendelee na shule kwa sababu mgogoro huu umekuwa ukijirudia mara kwa mara? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dorothy George Kilave, Mbunge wa Jimbo la Temeke, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nawaagiza Halmashauri ya Temeke kwamba baada ya rufaa hii kwisha, mara moja waanze mchakato wa kuweka mipaka halisi ili watu wasiende kuvamia hilo eneo. Kwa hiyo, mchakato uanze mara moja kuanzia sasa.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.