Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zahor Mohamed Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwera

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI aliuza: - Je, Serikali inaweza kutoa idadi na aina ya mikopo ya Zanzibar baada ya makubaliano na kuiwezesha Zanzibar kukopa yenyewe?

Supplementary Question 1

MHE. ZAHOR MOHAMED HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri naomba kuuliza maswali mawili ya ziada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza; je, Serikali sasa iko tayari kutoa taaluma hii baada ya mkanganyiko wa mambo haya kwa upande wa Zanzibar?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili; je, lini hili linaweza kuanza kufanyika kwa ajili ya kuondoa huo mkanganyiko? Ahsante.

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Zahor kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyo ada ya Serikali kutoa taaluma kwa wananchi wake na taasisi mbalimbali, Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi wote juu ya jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili anauliza, ni lini? Niseme, Serikali kutoa taaluma kwa wananchi wake ni suala endelevu. Kwa hiyo, tunaendelea kutoa taaluma kwa wananchi.