Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Muharami Shabani Mkenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuvisaidia vikundi vya BMU ili kuendeleza kasi ya upandaji mikoko na kusafisha fukwe kuanzia Pwani ya Bagamoyo, Pangani hadi Tanga?

Supplementary Question 1

MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, je, Waziri anaweza kutueleza ni mafanikio yapi yamepatikana katika mpango huo toka umeanza kutekelezwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Bagamoyo imekumbwa na changamoto kubwa sasa hivi ya kumegwa ardhi na maji ya bahari na hasa katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo na maeneo mengineyo.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha inadhibiti hali hiyo isiweze kuendelea.

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kujibu swali, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Muharami kwa juhudi yake ya ufuatiliaji wa mazingira lakini na mabadiliko ya tabianchi katika Jimbo lake la Bagamoyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio ambayo yamepatikana katika miradi hii, moja; ofisi tano za BMUs tumejenga katika Wilaya za Bagamoyo na Pangani. Sehemu ambazo zimejengewa ofisi hizo na kuzipatia samani ni pamoja na Saadani, Chalinze; Zingibari, Mkinga; Kipumbwi, Pangani; Dunda, Bagamoyo; na Sudimtama na tumewanunulia viatu na makato kwa ajili ya kusimamia usafi huu wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ni kweli kwamba Bagamoyo ni moja ya kati ya sehemu ambazo zina changamoto kubwa za mabadiliko ya tabianchi, lakini tayari ofisi yetu imeshapeleka watalaam kufanya upembuzi yakinifu na kufanya survey ambayo ni sahihi na watalaam hawa wameshaleta majibu, siku za karibuni hivi basi mradi utaanza kutekelezwa katika eneo hilo. Ahsante.