Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Josephat Mathias Gwajima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kawe

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza: - Je, Serikali haioni kuwa ni wakati muafaka wa kuzipandisha hadhi barabara za ndani za Jimbo la Kawe ili zihudumiwe na TANROADS kwa kuwa uwezo wa TARURA kuhudumia ni kilometa 120 wakati Jimbo lina barabara zenye jumla ya kilometa 1,463?

Supplementary Question 1

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina swali moja tu la nyongeza.

Kwa kuwa Jimbo la Kawe lina barabara nyingi sana ambazo zinaunganisha Wilaya na Wilaya kwa mfano, Wilaya ya Ubungo pamoja na Kindondoni huko kwa juu.

Ni lini sasa Waziri atakwenda pamoja nami ili ukaone hali halisi katika Jimbo hilo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MITAA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Askofu Josephat Mathias Gwajima, Mbunge wa Jimbo la Kawe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mara baada ya Bunge nitaongozana na wewe pamoja na wale Wabunge ambao niliahidi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuzungukia barabara zote za Mkoa huo, ahsante. (Makofi)