Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kusomesha Wahadhiri wengi zaidi katika ngazi ya Shahada ya Uzamivu (Ph.D) kwani waliopo sasa ni wachache?

Supplementary Question 1

MHE. DKT THEA M. NTARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri, kwa mara ya kwanza mimi naona amelitendea haki sana swali hilo, ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; ili kuendelea kupunguza uhaba wa wahadhiri;

Je, Serikali haiwezi kurudisha utaratibu wa kuwafanya wahadhiri hao wafundishe hata baada ya miaka 65 kama nchi nyingine za Marekani na Ujerumani?

Name

Prof. Joyce Lazaro Ndalichako

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kasulu Mjini

Answer

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Ntara kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la wahadhiri wetu kufundisha zaidi ya miaka 65 ni suala la kiutumishi kwenye kanuni zetu za kiutumishi. Nimuhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tunalichukua suala hili, tutakwenda kukaa na wenzetu wa Wizara ya Utumishi ili tuweze kuangalia namna gani ya kurekebisha sheria zetu zile ili ziendane sasa na mahitaji haya muhimu ya soko letu la wahadhiri nchini. Ahsante sana.