Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Primary Question

MHE. DANIEL B. SILLO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Bashnet baada ya Serikali ya Kijiji kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi huo?

Supplementary Question 1

MHE. DANIEL B. SILLO: Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri yanayotia moyo, lakini naomba niulize swali moja tu dogo la nyongeza.

Je, Serikali ipo tayari kuongeza wataalam wa afya katika Kituo cha Afya cha Ufana ambacho kipo jirani na Bashnet ili wananchi wa Bashnet wapate huduma ya afya wakati wanasubiri kujengewa kituo cha afya? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Daniel Baran Sillo, Mbunge wa Babati Vijijini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ipo tayari kuongeza watumishi katika kituo cha afya katika ajira hizi za watumishi 2,726 zilizotangazwa, ahsante sana. (Makofi)