Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Josephat Mathias Gwajima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kawe

Primary Question

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itakuja na mpango maalum wa kurasimisha makazi ya wananchi wa Mabwepande, Nakasangwe, Chasimba, Chatembo, Chachui, Ndumbwi na Jogoo ili kumaliza migogoro ya ardhi na kuiongezea mapato Serikali?

Supplementary Question 1

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, napenda kuuliza:-

Mheshimiwa Spika, huko Nyakasangwe ambapo kule nyuma kumetokea mauaji kwa sababu ya matatizo ya ardhi. Je, ni lini sasa Waziri atakwenda pamoja nami huko ili tushughulike kuweka mambo ya wananchi sawa? Ahsante sana.

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, napenda nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge, Askofu Gwajima, kwamba tutapanga wakati wowote tuweze kwenda kwa sababu sasa tuko kwenye bajeti, lakini tutapata fursa nzuri ya kwenda kwenye eneo alilolitaja.