Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara yenye kilometa 13 kuanzia Rau Madukani – Mamboleo – Shimbwe Juu katika Jimbo la Moshi Vijijini?

Supplementary Question 1

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kutokana na jiografia ya Mkoa wa Kilimanjaro, niseme ukweli kwamba changamoto yetu kubwa kule Kilimanjaro ni barabara hasa Jimbo langu la Moshi Vijijini na wakati wa mvua kama huu kuna mafuriko makubwa sana. Naomba nimuulize Naibu Waziri ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya TPC – Mabogini – Kahe yenye urefu wa kilometa 11.4 na kumalizia zile za Kibosho Shine - Kwa Raphael - International School - Kiboriloni - Sudini – Kidia?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Serikali ilishasema ingeanza upembuzi yakinifu wa barabara ya Uru – Mamboleo - Materuni yenye kilometa 10.2, ni lini Serikali itafanya zoezi hilo. Ahsante. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu maswali madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Profesa Patrick Alois Ndakidemi, Mbunge wa Moshi Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama ulivyoniongoza, umeniomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge kuhusu ni lini upembuzi yakinifu utaanza katika barabara ya Uru – Mamboleo – Materuni yenye urefu wa kilometa 10.2.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais makini kabisa Mama Samia Hassan Suluhu, tumesikiliza maombi ya Mheshimiwa Mbunge. Kwa sababu ameomba tu upembuzi yakinifu na nafahamu mpaka muda huu TARURA wananisikiliza ni agizo langu kwao kwamba sasa watenge fedha waanze upembuzi yakinifu kwa ajili ya barabara hiyo ili iweze kujengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia hizo barabara nyingine zote ambazo ameziainisha, Serikali imesikia tutaziweka katika Mpango kuhakikisha zinakamilika kwa wakati. Ahsante sana. (Makofi)