Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE (K.n.y. MHE. SILVESTRY F. KOKA) Aliuliza:- Miundombinu ya maji katika Shirika la Elimu Kibaha ilijengwa miaka 50 iliyopita kwa kutumia mabomba ya Asbestos ambayo siyo rafiki kwa afya za binadamu, lakini pia ni chakavu sana:- (a) Je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya maji katika shirika hilo? (b) Je, ni lini Serikali itakarabati majengo ya Chuo cha FDC katika Shirika hili?

Supplementary Question 1

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Halmashauri ya Jimbo la Kyerwa, tunalo jengo la halmashauri. Jengo hili limechukua muda mrefu na halijakamilishwa. Nini ahadi ya Serikali kukamilisha lile jengo la halmashauri katika Wilaya ya Kyerwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Innocent Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali ndiyo inayojenga majengo yote ya halmashauri katika nchi yetu likiwemo jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. Hivyo basi, kutokana na mahitaji na malengo ya Serikali ambayo imejiwekea na bajeti ambayo tumeitenga, tutalikamilisha lile jengo kadri bajeti yetu tulivyoiweka. Ahsante sana.