Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI (K.n.y. MHE. OSCAR R. MUKASA) aliuliza:- Kata ya Biharamulo Mjini imetangazwa kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo hivi karibuni; kwa sasa kuna mahitaji makubwa ya upangaji wa ardhi na makazi hasa katika hadhi ya kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo:- Je, Serikali ipo tayari kuwaunga mkono wananchi wa Biharamulo Mjini wakati huu ambapo wao wenyewe wanaendelea na jitihada za ndani kuhakikisha wanakuwa na upangaji wa makazi unaoendana na hadhi mpya ya Mamlaka ya Mji Mdogo?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, Mheshimiwa Waziri, hivi karibuni alikuja Lushoto ambako kulikuwa na tatizo la upangaji wa ardhi katika Mji Mdogo wa Mnazi ambapo pesa ambazo zimetumika vibaya nje ya utaratibu na ulitoa maagizo. Sasa nataka kujua ni kwa kiasi gani jambo lile Ofisi ya Rais, TAMISEMI imelishughulikia?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mji Mdogo wa Lushoto umeshatangazwa takribani miaka tisa, lakini mpaka sasa mamlaka ile bado haijaanza kazi, bado inapatikana ndani ya Halmashauri ya Lushoto. Sasa je, ni lini sasa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Lushoto itaanza kufanya kazi? (Makofi)

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, asante. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shangazi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli nilifanya ziara katika Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga na nikakuta kuna matumizi mabaya ya fedha shilingi zaidi ya milioni 300. Nikatoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya, namshukuru uchunguzi umeshafanyika, tumeshapokea taarifa ile watu wote waliohusika namhakikishia Mheshimiwa Mbunge watashughulikiwa kwa mujibu wa tararibu za kisheria, tunalifanyia kazi jambo hilo, naomba tupeane muda, tuvute subira kidogo.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa Mbunge anaulizia habari ya Mji Mdogo ambao ulitangazwa na haujawa mamlaka kamili. Nimejibu maswali haya mara kadhaa, nirudie tu kusema kwamba kama jambo hili haliongezi gharama za kuendesha Serikali, tumeelekeza na ni msimamo wa Serikali kwamba kwa sasa tujielekeze kuboresha maeneo na kukamilisha maeneo ambayo yalishaanzishwa kabla ya kuanzisha maeneo mengine ya mji.

Mheshimiwa Spika, sasa kama hili linaongeza gharama, kuongeza watumishi, majengo ya Serikali na bajeti kuongezeka, kwa kweli Serikali haitakuwa tayari kufanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hayo ndiyo majibu ya Serikali na Mheshimiwa Mbunge aendelee kutoa ushirikiano. Kadri tutakavyopata fedha ya kutosha, yale maeneo ambayo yameshaanzishwa yakaimarishwa vizuri kwa kupeleka huduma muhimu, vifaa, watendaji wa kutosha, basi maeneo mengine mapya yataanzishwa ili kupeleka huduma karibu na wananchi wetu. Ahsante.