Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Lucy Simon Magereli

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LUCY S. MAGERELI aliuliza:- Mwaka 2018 Serikali ilipitisha Sheria ya Udhibiti ya Taasisi Ndogo za Fedha SACCOS, VICOBA, Vikundi vya kuchangishana na kukopeshana, vyote vipate usajili na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania:- (a) Je, zoezi hili limeshatekelezwa kwa asilimia ngapi na ni taasisi ngapi zimesajiliwa? (b) Je, Serikali haioni kuwa zoezi hili ni over – regul ation na kuwanyima fursa ambayo imekuwa ikiwasaidia wakopaji na wakopeshaji wadogo kusaidiana katika jamii zao?

Supplementary Question 1

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Baada ya maelezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, natamani kufahamu, Serikali inafanya jitihada gani na kwa kutumia utaratibu gani kuhakikisha kwamba watumiaji wa huduma ndogo za fedha wanapata taarifa kuhusu hii sheria mpya, lakini hizi kanuni ambazo amezitunga pamoja na hiyo grace period ambayo wamewapa kabla ya kaunza utaratibu wa usajili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika majibu yake anasema lengo la kutungwa sheria hii ilikuwa ni kutatua changamoto ikiwemo ya utozaji wa riba kubwa lakini suala la utozaji wa riba kubwa si tu kwa sekta ndogo ya fedha hata huduma za fedha kwa ujumla wake kwa maana ya sekta rasmi kwa maana ya mabenki bado riba zinazotozwa ni kubwa sana. Je, Serikali inafanya nini kuhusu hili la ku-regulate hata riba ambazo zinatozwa na mabenki sasa hivi? (Makofi)

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Lucy Simon Magereli, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza jitihada na utaratibu ambao Serikali tunatumia kufikisha taarifa ni kwamba tunaendesha makongamano sehemu mbalimbali, ndiyo maana kwenye jibu langu la msingi nimesema kwamba tumewashirikisha walengwa wote katika katika makundi yote manne yaani kuanzia tier one to tier four, wote wameshirikishwa tulipokuwa tunaandaa kanuni hizi za ujumla za Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Pia kanuni maalum kwa ajili ya daraja la pili mpaka daraja la nne, tumekaa na makundi mbalimbali, tumeendesha semina na warsha mbalimbali. Tunapokamilisha kuandaa kanuni hizi ambazo tayari zimeshatolewa tarehe 2 Agosti, tutaendelea kuwatembelea wenye taasisi hizi ili tuweze kuwafikia kwa ujumla na wawe na uelewa wa pamoja wa dhamira njema ya kuandaa Sera yetu ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 pamoja na sheria yake ya mwaka 2018 na kanuni zake zote mbili za mwaka 2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, naomba kumwambia Mheshimiwa Lucy kwamba riba inayotozwa katika sekta rasmi ya taasisi za fedha siyo kubwa. Nakumbuka wakati tulipoingia madarakani mwaka 2015, riba ilikuwa kuanzia asilimia 21 hadi asilimia 25, lakini kwa sasa katika taasisi ambazo ni rasmi za kifedha, pamoja na jitihada kubwa zilizochukuliwa na Benki Kuu ya Tanzania ya kushusha discount rate pamoja na amana inayotakiwa kuwekezwa Benki Kuu, riba ni kuanzia asilimia 15 hadi asilimia 17.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuliambia Bunge lako Tukufu kwamba mabenki haya au taasisi hizi za fedha wanapo-set riba hii, huwa wanaangalia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na gharama wanazozitumia katika kutoa huduma hizi. Serikali tunajitahidi sana kusimamia taasisi hizi za kifedha ili kuhakikisha eneo moja ambalo lilikuwa likichangia riba kuwa juu nayo ni administration inakwenda chini, administrative cost ishuke ili riba iendelee kushuka kwa faida ya Watanzania na uchumi wetu kwa ujumla.