Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Janet Zebedayo Mbene

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ileje

Primary Question

MHE. JANET Z. MBENE Aliuliza:- Geological Surveys za Wilaya au Mikoa mingi ni za miaka mingi tangu enzi za ukoloni. Surveys hizi nyingi zimejikita kwenye aina moja ya migodi kwa mfano Mkoa wa Songwe Survey imezungumzia machimbo ya mawe peke yake:- (a) Je, ni lini Serikali itafanya mapitio ili kupata Geological Surveys zenye kujumuisha aina nyingine za madini ambayo yanapatikana katika Mkoa wa Songwe hususan Ileje? (b) Je, Serikali ipo tayari kwenda kuwaelimisha wananchi wa Ileje juu ya madini yaliyopo na kuhamasisha uwekezaji kwa wachimbaji wadogo?

Supplementary Question 1

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Naibu Waziri kwa majibu ingawa ningefurahi zaidi yangekuwa siyo ya kijumla kiasi hicho kwa sababu ningependa japo nisikie tu kuwa kama wapo tayari kuja kufanya hata mafunzo tu kwa ajili ya vijana wetu ambao wanajishughulisha na shughuli hizi. Hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza:

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ni kuhusiana na ule Mgodi wa Kiwira ule waunderground. Mgodi ule umesimama kwa muda mrefu sana na hivi sasa tunavyozungumza hatuna hakika yaani kuna sintofahamu ya kujua ni nani mwekezaji na lini ataanza kufanya kazi ili tuweze kuona mafanikio ya mgodi ule?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kuwa mwaka 2010 Kamati ya Kudumu ya Bunge ilishauri kuwa mgodi ule uwekwe chini ya STAMICO na TANESCO kwa sababu madhumuni ya mgodi ule ilikuwa ni kuzalisha umeme, lakini mpaka sasa hivi tunaona uko chini ya STAMICO lakini hatuoni ule ubia na TANESCO ambao ungesaidia sasa katika kuhakikisha kuwa umeme unapatikana? Ahsante.

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa kwamba ule Mgodi wa Kiwira umesimama kwa muda mrefu sasa na tatizo lilikuwa ni moja tu, baada ya ile kampuni ya TAN Power Resources kutoka pale ilitakiwa kwamba wahamishe zile share zao ili ziweze kuchukuliwa na Serikali na share hizo tungeweza kuzipeleka STAMICO kwa ajili ya kuanzisha au kuendeleza mradi ule.

Sasa wale TAN Power Resources walikuwa na deni ambalo walitakiwa walipe (capital gain tax)ambayo ilikuwa ni deni la bilioni 2.9 hawajalipa lile deni na Serikali kupitia TRAni kwamba wanafatilia kuweza kuwabana wale wahusika waweze kulipa deni hilo ili tuweze kupata tax clearance na kuhamisha zile share ziweze kwenda Serikalini au STAMICO ili kuweza kuanzisha mradi ule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi TRA wanaendelea kufatilia hawa TAN Power Resources na inasemekana hawapo na watu hawa ambao hawapo sasa hivi kuna hatua inayofuata ya kufatilia kuwajua ma-director wa ile TAN Power Resources na kuweza kuwabana ikiwezekana kwenda kuchukua passport zao binafsi ili waweze kulipa lile deni la 2.9 bilioni. Baada ya kufanya hivyo STAMICO wakishachukua mradi huo mara moja mradi ule utaanza na uchimbaji utaendelea. Ahsante sana.