Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Musa Rashid Ntimizi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igalula

Primary Question

MHE. MUSA R. NTIMIZI aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Tura katika Vijiji vya Mwamlela, Mmunyu na Nkongwa hawana kabisa mawasiliano ya simu licha ya umuhimu wa mawasiliano kiusalama na kiuchumi:- Je, Serikali inatoa ahadi gani ya kupatikana kwa mawasiliano katika vijiji hivyo?

Supplementary Question 1

MHE. MUSA R. NTIMIZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kumekuwa na kawaida ya hawa service providers pamoja na ruzuku wanayopata kutoka Serikalini kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote wamekuwa wanajikusanya kwenye maeneo ambayo tayari kuna mawasiliano badala ya yale madhumuni ya kupeleka mawasiliano kwenye maeneo ambayo hayana mawasiliano. Mfano katika jibu lake la swali langu, katika Kata ya hiyo ya Tura, Kijiji cha Karangasi, tayari kuna mawasiliano lakini bado tena kumepelekwa mtandao mwingine, lakini yapo maeneo ambayo hayana mawasiliano. Je, kwa nini sasa hawa Service Providers wasipeleke mawasiliano kwenye maeneo yale ambayo hayana mawasiliano?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Kata ya Mmale yote haina mawasiliano; je, ni lini Serikali itapeleka mawasiliano katika Kata hiyo ya Mmale? (Makofi)

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge wa Tura kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, hoja yako uliyoizungumza ni kweli, kwamba service providers, watoa huduma za mawasiliano walikuwa wanajirundika kwenye maeneo machache, maeneo ambayo yana biashara kubwa au yana population kubwa ya watu. Baada ya kuliona hili, Bunge hili hili liliamua kuunda Mfuko wa Masiliano kwa Wote. Maana yake nini, ni kwamba ule Mfuko sasa unaenda kwenye maeneo yale ambayo, hawa wanaofanya biashara tu bila kujali utu wa mwanadamu Mtanzania, kwamba sasa tuwalazimishe waende kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko huu tayari, sasa hivi tunaenda maeneo yote bila kujali kwamba kuna faida kubwa na ndiyo maana hata kwenye maeneo anayoyahitaji Mheshimiwa Mbunge sasa, baada ya kutangaza hii tenda tutahakikisha kata zote, maeneo yote ili mradi yana Watanzania yanapata huduma ya mawasiliano. (Makofi)